Wednesday, 15 February 2017

UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.

UTAYARISHAJI WA CHAKULA CHA KUKU.

Ili kuku akue vizuri na haraka anahitaji chakula bora na kilichokamili.
√ Kwa vifaranga wapewe chakula chao (Chick Mash).
√ Bloiler mash kwa ajili ya kuku wa nyama
√ layer mash kwa ajili ya kuku wa mayai.
√ Grower mash kwa ajili ya kuku wanaokua
√ breeder mash kwa ajili ya kuku wazazi. Chakula hiki kinafaa sana kwa kuku wa kienyeji wanaofugwa kisasa.

Mahitaji ya kuandaa chakula cha kuku.

1: Layer mash.
-Mahindi kg 40
-Pumba za mahindi kg 10
-Pumba za mpunga kg 10
-Mashudu ya pamba kg 5
-Mashudu ya alizeti kg 15
-Dagaa kg 8
-Chokaa kg 8
-Unga wa mifupa kg 3
-Chumvi kg 0.5
Output yake ni kgs 120-140
2: Chick Mash, Growers mash na Bloilers mash
-Mahindi kg 40
-Pumba za mahindi kg 10
-Mahindi aina ya paraza kg 10
-Pumba za mpunga kg 10
-Mashudu ya pamba kg 5
-Mashudu ya alizeti kg 18
-Mashudu ya nazi kg 1.5
-Dagaa kg 10
-Chokaa kg 8
-Unga wa mifupa kg 1.2
-Chumvi kg 0.5
-Damu kg 1.3
-Vitamin/Mineral prex kg 0.3
Output yake ni kgs 150-200
Peleka mashine na upate mchanganyo kamili wa mahindi na vingine visage kawaida kupata punje ili iwe rahisi kwa kuku kuweza kudonoa.

ULISHAJI WA KUKU
1. Vifaranga wa nyama
• Wapewe chakula cha vifaranga kwa wiki 3 (Starter)
• Wapewe chakula cha kumalizia kwa wiki 3 (Finisher).
2. Vifaranga wa mayai
• Wapewe chakula cha vifaranga kwa wiki 8 (Starter)
• Kuanzia wiki ya 9 kuku wapewe chakula cha kukuzia Growers mash mpaka wiki ya 18.



No comments:

Post a Comment